Go to Allah Before its to Late
- Fajr:3:25 am
- Dhuhr:12:04 pm
- Asr:5:00 pm
- Maghrib:7:06 pm
- Isha'a:8:45 pm
90: سورة البلد
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
In the Name of Allah—the Most Compassionate, Most Merciful.
lā uq'simu bihādhā l-baladi
Mwenyezi Mungu Anaapa kwa mji huu mtakatifu wa Makkah.
wa-anta ḥillun bihādhā l-baladi
Na wewe, ewe Nabii, ni mkazi wa mji huu mtakatifu.
wawālidin wamā walada
Na Anaapa kwa mzazi wa wanaadamu, ambaye ni Ādam, amani imshukie, na kilichozalikana na yeye.
laqad khalaqnā l-insāna fī kabadin
Hakika Tumemuumba binadamu katika usumbufu na shida za kilimwengu.
ayaḥsabu an lan yaqdira ʿalayhi aḥadun
Kwani anadhani kwa mali aliyoyakusanya kuwa Mwenyezi Mungu Hatakuwa na uwezo juu yake?
yaqūlu ahlaktu mālan lubadan
Huwa akisema kwa kujigamba: «Nimetumia mali mengi.»
ayaḥsabu an lam yarahu aḥadun
Kwani anadhani, kwa kitendo chake hiko, kuwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na kushinda, Hamuoni wala hatamhesabu juu ya kubwa na dogo?
alam najʿal lahu ʿaynayni
Kwani hatukumpa macho mawili ya kuonea,
walisānan washafatayni
ulimi na midomo miwili ya kusemea
wahadaynāhu l-najdayni
na kumfafanulia njia mbili: ya kheri na ya shari?
falā iq'taḥama l-ʿaqabata
Basi ajiepushe na janga la Akhera kwa kutoa mali yake ili aokoke.
wamā adrāka mā l-ʿaqabatu
Ni kitu gani kilichojulisha ni lipi hilo janga la Akhera na ni mambo gani yenye kusaidia kujiepusha nalo?
fakku raqabatin
Ni kuacha huru shingo iliyoamini kuikomboa na utumwa.
aw iṭ'ʿāmun fī yawmin dhī masghabatin
Au kulisha, wakati wa shida ya njaa,
yatīman dhā maqrabatin
yatima mwenye ujamaa, ili ipatikane fadhila ya sadaka na ya kuunga kizazi,
aw mis'kīnan dhā matrabatin
au masikini asiyekuwa na kitu.
thumma kāna mina alladhīna āmanū watawāṣaw bil-ṣabri watawāṣaw bil-marḥamati
Kisha akawa, baada ya kufanya amali njema zilizotajwa, ni miongoni mwa waliotakasa Imani yao kwa Mwenyezi Mungu, wakausiana kusubiri juu ya kumtii Mwenyezi Mungu kwa kufuata maamrisho Yake na kujiepusha na vitendo vya kumuasi na wakausiana kuwahurumia viumbe.
ulāika aṣḥābu l-maymanati
Wenye kufanya hayo ndiwo watu wa kulia ambao watapelekwa Siku ya Kiyama upande wa kulia kuelekea Peponi.
wa-alladhīna kafarū biāyātinā hum aṣḥābu l-mashamati
Na wale waliokanusha Qur’ani ndio ambao watapelekwa, Siku ya Kiyama, upande wa kushoto kuelekea Motoni.
ʿalayhim nārun mu'ṣadatun
Malipo yao ni Moto wa Jahanamu wenye kuwafinika na kuwaziba.
QuranQari.Pk